.

Chanzo cha picha, EPA

Takriban wanajeshi 200 wa Marekani ambao tayari wako Mashariki ya Kati watapelekwa Israel ili kusaidia kufuatilia usitishaji mapigano Gaza, kwa mujibu wa maafisa wa Marekani.

Jeshi la Marekani litaanzisha kikosi kazi cha kimataifa nchini Israel, kinachojulikana kama kituo cha uratibu wa kijeshi wa kiraia, ambacho huenda kikajumuisha wanajeshi kutoka Misri, Qatar, Uturuki na UAE, walisema.

Afisa mmoja mkuu alisema hakuna vikosi vya Marekani vitaingia Gaza, akiongeza kuwa jukumu la Marekani lilikuwa kuunda Kituo cha Udhibiti wa Pamoja ambacho “kitaunganisha” kikosi cha kimataifa kinachoingia.

Kikosi kazi hicho kitaongozwa na Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) yenye makao yake makuu katika eneo hilo, na inanuiwa kusimamia makubaliano ya kusitisha mapigano na pia kusaidia kuratibu misaada ya kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *