Shambulio hilo pia limeharibu barabara muhimu ya kuiunganisha mji wa Beirut na sehemu za kusini mwa Lebanon. 

Rais Aoun amesema kwa mara nyengine tena Lebanon imeendelea kuvamiwa vibaya na Israel bila ya uhalali wowote.

Nayo wizara ya afya nchini humo imesema shambulizi hilo katika kijiji cha Msayleh lililenga eneo kunakouzwa silaha nzito na kuharibu idadi kubwa ya magari. Israel yenyewe imekiri kushambulia kusini mwa Lebanon ikisemamashambulizi yake yamelenga miundombinu ya Hezbollah.

Israel imeendelea kuishambulia Lebanon licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini Mwezi Novemba mwaka jana yaliyofikiwa baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mashambulizi kati yake na wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *