
Hii ni baada ya baada ya Israel na Hamas kutia saini awamu ya kwanza ya kusitisha mapigano katika Ukanda huo.
Lakini bado kuna masuali mengi ya kujibiwa kuhusu ufanikishwaji kamili wa mpango wa amani ya Gaza wa rais wa Marekani Donald Trump.
Shirika la habari la Reutes lilielezea kuona idadi kubwa ya watu wakitembea kwa miguu kuelekea Gaza City.
Khalil Al-Deiri, ni mmoja wa wapalestina wanaorejea nyumbani.
“Tunatumai utakuwa usitishaji vita wenye baraka, wakati wa usalama na amani kwa watu wote. Tunatumai kwamba watu wote, raia wote wa mji wa Gaza, wataweza kurejea nyumbani.”
Msemaji wa ulinzi wa raia wa mji huo Mahmud Bassal amesema takriban wapalestina 200,000 wamerejea Kaskazini mwa Gaza tangu makubaliano hayo ya awamu ya kwanza ya kusitisha vita kutiwa saini kati ya pande hizi mbili hasimu.
Makubaliano hayo, yaliyotiwa saini nchini Misri yanafuatia mpango wa amani wa Gaza wenye vipengele 20 uliotangazwa mwezi uliopita na Rais wa Marekani Donald Trump, baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita vilivyochochewa na shambulio la kundi la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel.