Afisa huyo amesema hili ni shambulizi la hivi karibuni la Urusi kulenga mfumo wake wa nishati kuelekea kipindi cha baridi.

Hata hivyo serikali haikusema ni watu wangapi walioathirika na tukio hilo, lakini Kampuni kubwa kabisa ya kibinafsi ya nishati nchini Ukraine, DTEK,  iliripoti kukatika kwa umeme katika sehemu kubwa ya mji mkuu Kiev. 

Baadae Kampuni hiyo ilithibitisha kurejesha huduma hiyo kwa zaidi ya nyumba 240,000 katika eneo hilo.

Urusi imekuwa ikilenga mtandao wa nishati wa Ukraine kila mwaka wakati wa kipindi cha baridi, tangu ilipoanza uvamizi wake wa kijeshi kwa jirani yake huyo mwaka 2022, hatua iliyosababisha kukatika kwa umeme na mashini za kuongeza joto kwa mamilioni ya waukraine pamoja na kusambaratisha usambazaji wa maji jambo ambalo Ukraine inasema ni sawa na uhalifu wa kivita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *