Gwaride hilo la kijeshi lilianza jana Ijumaa (10.10.2025), wakati wa maadhimisho ya miaka 80 ya chama tawala cha wafanyakazi.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev, pamoja na Kiongozi mkuu wa chama cha kikomunisti cha Vietnam To Lam walionekana pembeni mwa Kim wakati akiongoza gwaride hilo.

Kim Jong Un wiki hii alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Li Qiang mjini Pyongyang na kusifu “uhusiano wa kirafiki na ushirikiano” wa nchi hizo mbili.

Ziara ya Li nchini humo imekuja wakati majirani hao wakitaka kudumisha uhusiano wa karibu licha ya muda wa uhusiano mbaya kati ya China na Korea Kaskazini kuhusu mpango wa nyuklia wa Pyongyang.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *