Kamati ya upinzani inayolipinga kundi la wanamgambo la RSF imesema kundi hilo ambalo limekuwa vitani na serikali ya Sudan tangu mwezi Aprili mwaka 2023 lililenga kambi ya  Dar al-Arqam katika chuo kikuu cha Omdurman na kusababisha mauaji ya watu 53 wakiwemo watoto 14 na wanawake 15.

Inasemekana bado miili imebakia chini ya vifusi vya jengo hilo. Kamati hiyo imelielezea tukio hilo kama mauaji ya halaiki na kutoa wito kwa jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati.

Kundi la RSF hadi sasa halijatoa tamko lolote juu ya shambulio hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *