Siku chache kabla ya Mgombea Urais wa CCM Dkt. SAMIA Suluhu Hassan kuwasili Mkoani Geita, Wanawake na Samia Mkoani humo wamefanya matembezi ya Amani na Kufanya uhamasishaji wa amani kuelekea uchaguzi na kuwasihi Wananchi kuendelea kumuamini Dkt. Samia na kumpokea kwa kishindo.
Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoani humo Bi Adelina Kabakama amesema lengo la tukio la leo ni kuwahimiza Wana Geita kupiga kura Kwa wingi na kulinda amani ya taifa.
Makamu Mwenyekiti wa Wanawake na SAMIA Geita Bi Mariam Kimwinyi ameonya uhamasishaji wa vurugu kuwa utakuwa na madhara makubwa Kwa Taifa.
Kw upande wake Mgombea viti Maalumu CCM Geita ambaye anawakilisha UWT Bi Regina Mikenze amewataka Wanawake kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Dkt. Samia kutokana na Kazi kubwa aliyofanya tangu apate nafasi hiyo baada ya kifo Cha RAIS awamu ya Tano DKT John MAGUFULI.
#StarTvUpdate