Siku moja kabla ya uchaguzi wa urais nchini Cameroon, serikali imefanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Oktoba 10, ili kusisitiza sheria kuhusu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi. Ikirejelea kwamba ni Baraza la Katiba pekee ndilo lililoidhinishwa kutangaza matokeo ya uchaguzi, pia imebainisha kwamba hakuna ukiukwaji wa kanuni utakaovumiliwa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati maandalizi ya mwisho ya uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, Oktoba 12 nchini Cameroon yakiendelea, Waziri wa Mambo ya Ndani, Paul Atanga Nji, amekumbusha siku ya Ijumaa kuhusu sheria kuhusu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi. Akitoa onyo kwa yeyote anayepanga kutangaza matokeo ya uchaguzi baada ya kupiga kura, almeishia kuwakamata wanaokiuka sheria hii.

Paul Atanga Nji amedai kuwa na habari kuhusu kuwepo kwa majukwaa yaliyokusudiwa kutangaza matokeo kabla ya tarehe iliyopangwa na nje ya saa rasmi za kupiga kura, akishtumu vitendo vya “kutowajibika, hatari na uhalifu”. Akiwalenga hasa wagombea wa upinzani, ametangaza kuwa serikali halitasita kuwachukulia hatua kali na kuwakamata ikibidi, na kuongeza kuwa makazi ya wagombea hayana milango iliyoimarishwa ya kuzuia risasi kuingia.

Kwa njia ya wazi zaidi na ya kutisha, Paul Atanga Nji pia amewaambia kwamba hadhi yao haitoi “kinga,” anaripoti mwandishi wetu wa Yaoundé, Polycarpe Essomba. Kauli hii hadi sasa imejibiwa tu na Profesa Abah Oyono. Masharti ya kisheria katika kanuni za uchaguzi hulinda ufichuzi wa hadharani wa matokeo ya kila kituo cha kupigia kura baada ya kuhesabu kura, amesema mshauri huyu wa karibu wa mgombea Issa Tchiroma Bakary, ambaye wengi wanamwona mlengwa mkuu wa onyo la mamlaka.

“Hatuna haki ya kufichua hata matokeo ya kituo kimoja cha kupigia kura”

Kuhusu vyombo vya habari, kazi ya waandishi wa habari pia inadhibitiwa sana. Ingawa ni wachache kati yao walioidhinishwa kuingia katika vituo vya kupigia kura, pia hawaruhusiwi kushiriki matokeo ya hesabu ya kura katika kituo kimoja au zaidi wanakosimamia uchaguzi.

“Hatuna haki ya kufichua hata matokeo ya kituo kimoja cha kupigia kura: mwandishi lazima ajiwekee kikomo katika kufanya uchaguzi uwe hai kwa wasikilizaji, lakini amepigwa marufuku kabisa kufichua tokeo moja,” analalamika Emmanuel Koko, mwandishi wa habari katika Balafon Media, ambaye ataendesha kazi yake kuhusianana uchaguzi huo huko Garoua. “Hii ni aibu kwa sababu jirani kabisa na sisi, Nigeria, wanapiga kura asubuhi na kupata matokeo jioni. Nchini Cameroon, inachukua wiki mbili!” ameongeza, akihojiwa na mwandishi wetu maalum huko Douala, Amélie Tulet.

Ingawa hata Élécam, tume inayoandaa uchaguzi, haitoi matokeo yoyote ya sehemu au ya muda, David Moukoudi, mwanachama wa shirika lisilo la kiserikali la Un monde avenir, anaona utaratibu huu kama utaratibu wa udanganyifu wa uchaguzi: “Kwa hiyo, kwa vile hakuna matokeo ambayo bado ni ya umma, hakuna mtu anayeweza kupinga matokeo kutoka kwa kituo fulani cha kupigia kura. Na kwa kuwa chombo pekee kilichoidhinishwa kutangaza ni Baraza la Kikatiba ambalo haliwezekani, kwa hivyo mara baada ya kuyatoa, yanakuwa ni yamoja kwa moja, hakuna kurekebisha au kubadilisha chochote”, analaani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *