
Chanzo cha picha, Reuters
Kundi la
Hamas limewaita wanachama wapatao 7,000 wa vikosi vyake vya usalama kudhibiti
tena maeneo ya Gaza ambayo yameachwa hivi karibuni na wanajeshi wa Israel, kwa
mujibu wa vyanzo vya ndani.
Kundi hilo pia
liliteua magavana wapya watano wote wenye asili ya kijeshi, ambao hapo awali
waliongoza brigedi.
Amri hiyo imeripotiwa
kutolewa kupitia simu na ujumbe mfupi ambao ulisema lengo lilikuwa “kusafisha Gaza dhidi ya wahalifu na washirika na Israeli” na kuwataka
wapiganaji kuripoti ndani ya masaa 24.
Ripoti
kutoka Gaza zinaonyesha kuwa vikosi vya Hamas vyenye silaha tayari vimesambazwa
katika wilaya kadhaa, baadhi wakiwa wamevalia nguo za kiraia na wengine katika
sare za bluu za polisi wa Gaza.
Mvutano
uliongezeka sana na haraka baada ya wanachama wawili wa vikosi vya wasomi wa
Hamas kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha kutoka ukoo wenye nguvu wa
Dughmush katika kitongoji cha Sabra katika mji wa Gaza.
Mmoja wao
alikuwa mtoto wa kamanda mkuu katika mrengo wa kijeshi wa Hamas, Imad Aqel,
ambaye sasa anaongoza ujasusi wa kijeshi wa kundi hilo.
Miili yao
iliachwa barabarani, na kusababisha hasira na kuongeza matarajio ya Hamas
kujibu.
Wanachama wa
Hamas baadaye walizingira eneo kubwa ambapo zaidi ya wapiganaji 300 wa kundi la
Dughmush waliaminika kuwa wamejificha huku wakiwa na bunduki na vilipuzi.
Jumamosi
asubuhi, Hamas ilimuua mtu mmoja wa ukoo wa Dughmush, na inasemekana kuwateka
nyara wengine 30.
Soma zaidi: