
Chanzo cha picha, Getty Images
Miongoni mwa vyakula kama wali,Chapati,mkate viazi na viazi vitamu huwa kuna walau aina moja au zaidi ya vyakula tunavyovipenda zaidi.
Hii ndio maana tafiti zimebaini kwamba lishe ya kihindi huwa na kiasi kikubwa zaidi cha wanga duniani.Na kuongeza kwamba hii ndio sababu kuu ya kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha wagonjwa wa kisukari na watu wenye uzito uliopitiliza miongoni mwa wahindi.
Utafiti huu uliofanywa na Baraza la India la Utafiti wa tiba na Ugonjwa wa Kisukari (ICMR-IndiaB) umefichua mambo mengi muhimu.
Wahindi wanapata wapi kalori nyingi na ni mabadiliko gani yanahitajika kufanywa katika lishe yetu?
Baraza la India la Utafiti wa Matibabu na Ugonjwa wa Kisukari wamefanya utafiti juu ya lishe ya Wahindi.
Utafiti huo, ulioitwa “Dietary Profile and Associated Metabolic Risk Factors in India from the ICMR-IndiaB Survey-21”, umechapishwa katika jarida la sayansi linaloitwa Nature.
Kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari, uzito kupita kiasi
Jumla ya watu 1,21,077 kutoka majimbo, maeneo ya mji mkuu Delhi walihusishwa katika utafiti huo.
Utafiti huu unaonesha kuwa asilimia 62 ya kalori zote zinazotumiwa na Wahindi zinatokana na wanga (carbohydrates).
Miongoni mwao, ulaji wa vyakula vyenye kabohaidreti duni, kama vile wali mweupe, nafaka zisizokobolewa, na sukari iliyoongezwa, kama vile sukari, asali, siagi na sukari ya mawese, kwa kiasi kikubwa.
Hakika kuna mwelekeo wa kikanda katika mlo wa Kihindi. Mchele ni chakula kikuu katika sehemu za kusini, mashariki, na kaskazini mashariki mwa India.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ngano ndicho chakula kikuu katika maeneo ya Kaskazini na Katikati mwa India. Mtama ndio nafaka zenye lishe zaidi, lakini ni majimbo matatu tu, Karnataka, Gujarat na Maharashtra, ambayo hujumuisha nafaka mbichi katika lishe yao ya kila siku.
Matumizi ya sukari ni makubwa kote nchini humo. Inapendekezwa kutumia si zaidi ya 5% ya kalori kila siku kutoka kwenye sukari. Lakini katika majimbo 21 na maeneo mengine, kiasi hiki ni zaidi ya 5%.
Hii inasababisha kuongezeka kwa wagonjwa wa kisukari au kuongezeka kwa watu wenye uzito uliopitiliza.
Ingawa kiasi cha mafuta katika vyakula vya Kihindi kiko ndani ya kiwango,bado ulaji wa mafuta mengi upo kila mahali isipokuwa katika majimbo ya Jharkhand, Chhattisgarh, Arunachal Pradesh na Manipur.
Ulaji wa protini ni mdogo kuliko ilivyotarajiwa
Suala zito ni kwamba ulaji wa protini kote nchini ni mdogo kuliko ilivyotarajiwa.
Kwa wastani, 12% tu ya kalori ya kila siku hutoka kwa protini. Protini nyingi hutoka kwa nafaka, kunde, na nafaka. Bidhaa za maziwa huchangia 2% na ulaji wa protini za wanyama ni 1% tu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Majimbo ya Kaskazini-mashariki yana kiwango cha juu cha protini katika lishe yao.
Kwa hiyo kinachotokea kwa haya yote ni kwamba mlo usio na usawa umeongeza matukio ya watu kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Ina matukio mengi ya watu kupata magonjwa wa moyo, kisukari, shinikizo la damu, na uzito uliopitiliza. Ulaji mwingi wa wanga huongeza hatari ya kisukari, viashiria vya awali vya kisukari uzito uliopitiliza kwa 15-30%.
Kwa hivyo ni nini cha kifanyike?
Wataalamu wanasema kuwa karibu asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kuzuiwa kwa kuboresha lishe na kufanya mazoezi ya mwili.
Sasa, watafiti wameeleza kwamba iwapo tutapunguza kalori zinazotokana na wanga kwa asilimia 5, na kuongeza kwa asilimia 5 ulaji wa protini inyaotokana na mimea na bidhaa za maziwa, hatari ya kupata kisukari au viashiria vya awali vya kisukari (pre-diabetes) inaweza kupunguzwa kwa kiwango kikubwa.