Zelensky amesemaUrusi imeweza kuzidisha mashambulio inayoyafanya kwa sababu dunia imeelekeza kipaumbele katika kuhakikisha amani ya Mashariki ya Kati.

Dunia yapaswa kuongeza shinikizo kwa Urusi

Rais wa Ukraine amesema dunia haipaswi kulegeza shinikizo na kwamba inapasa kuendeleza vikwazo, ushuru, na hatua za pamoja dhidi ya wale wanaonunua nishati kutoka Urusi. Wakati huo huo jeshi la anga la Ukraine limeripoti mashambulio mengine 100 yaliyofanywa na Urusi hii leo kwa kutumia droni. Katika mashambulio hayo Urusi imeilenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine. Miji kadhaa ya kusini, kaskazini na masharikimwa nchi hiyo imeshambuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *