Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka amewashangaa watu wanaobeza anachofanya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kumnadi mgombea wa uras, Samia Suluhu Hassan.
Ole Sendeka amesema hayo leo Jumapili Oktoba 12,2025 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha na kuongeza kuwa anachofanya kiongozi huyo ni utaratibu uliokuwepo tangu enzi na enzi.
“Kikwete alimnadi mgombea urais, John Magufuli na ikaonekana sawa, iwaje leo akisimama kwa ajii ya mgombea wa sasa DKt Samia iwe nongwa’,” amesisitiza Ole Sendeka ambaye pia ameshika nafasi mbalimbali ikiwamo Nkuu wa Mkoa wa Njombe na mbunge wa Simanjiro.
#StarTvUpdate