Kwa sasa Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miradi 13 ya dharura katika mkoa wa Lindi ambayo itatumia jumla ya shilingi Bilioni 119 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya dharura.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Daraja la Kipwata (Mita 40) na Boksi kalavati eneo la Sakura na Songas, Ujenzi wa Daraja la Mikereng’ende (mita 40) na Boksi kalavati katika maeneo ya Mtandango/Stakshari na Masaninga, Ujenzi wa Boksi kalavati la Mbwemkuru I (seli 4, 5m x 4m), na matuta ya kuzuia mmomomnyoko wa udongo ( Spur dykes), Ujenzi wa Daraja la Somanga Mtama (60m) na Ujenzi wa Daraja la Njenga II (60m) ambapo miradi yote hii ipo katika barabara Kuu ya Marendego – Lindi – Mingoyo
Miradi mingine ni Ujenzi wa Daraja la Miguruwe (39m) pamoja na Boksi kalavati nne (4), Ujenzi wa Daraja la Zinga (18m) na Ujenzi wa Daraja la Kimambi (39m) ambayo ipo katika Barabara ya Mkoa ya Nangurukuru – Liwale.
Fedha hizo zinaendelea na utekelezaji wa miradi ya Barabara ya Mkoa ya Liwale – Nachingwea ambayo ni Ujenzi wa Daraja la Nangano (20m) na Makalavati ya Dharura ya mawili ya vipimo 2×2, mawili ya vipimo 5×2.5, Ujenzi wa Daraja la Mbwemkuru II (64m). Katika Barabara ya Mkoa ya Kiranjeranje- Namichiga serikali inaendelea na Ujenzi wa Daraja la Nakiu (70m) na Ujenzi wa Daraja la Kigombo (25m) na kalavati ya vipimo vya 5×4 huku katika Barabara ya Mkoa ya Tingi – Kipatimo Ujenzi wa Makalavati sita (6) ukiwa unaendelea.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa miradi hiyo Msimamizi wa kitengo cha miradi ya Maendeleo TANROADS Mkoa wa Lindi Mhandisi Fred Sanga amesema kuwa mpaka sasa jumla ya shilingi Bilioni 58.5 zimeshalipwa kwa mkandarasi na kazi inaendelea kwa kasi ambayo itakamilika Disemba mwaka huu.
#StarTvUpdate