Maandamano dhidi ya serikali nchini Madagascar yanazidi kuongezeka. siku ya Jumamosi, Oktoba 11, makundi ya wanajeshi yamejiunga na maandamano katika mitaa ya Antananarivo, na kikosi cha jeshi la Madagascar kimetoa wito wa “kukataliwa kwa amri ya kuwapiga risasi” waandamanaji. Shinikizo linaongezeka kwa Rais Andry Rajoelina.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Madagascar, baada ya siku 17 za maandamano ya vuguvugu la vijana la Gen Z, wanajeshi wameamua kujiunga na waandamanaji na kutoa wito wa kutotii serikali. Hali ilibadilika siku ya Jumamosi, Oktoba 11, kwa video hii, ya zaidi ya dakika nane, ambapo Kanali Mickaël Randrianirina anatoa wito wa kutotii serikali.

“Tunaweza kufikiri kwamba jeshi limechukua msimamo wa wazi wa kisiasa…”, anasema Christiane Rafidi-Nariv, mtalamu wa masuala ya siasa na mtafiti mshiriki katika Cevipof

“Iwapo rais hataondoka, hali hii itamalizika kwa umwagaji damu,” anahofia Benja kwenye Place du 13-Mai.

Baada ya magari mawili ya kivita kuondoka katika kambi ya kijeshi ya Capsat, maelfu ya waandamanaji walikusanyika Jumamosi alasiri kwenye eneo la Mei 13, katikati mwa Antananarivo.

Benja, mfanyakazi aliyejiajiri baada ya mauzo, alitoa shukrani zake kwa wanajeshi waliotoa wito wa kutotii:

“Nawashukuru kwa kuwaunga mkono wananchi, wao pia ni sehemu yao, wana familia, na wanajua tunayopitia. Leo imeweka historia kweli kweli, kwa sababu kama hawangekuwepo, kwa bahati mbaya, mgomo wa amani haungefanikiwa. Shukrani kwa jeshi, tumeweza kufika eneo la Mei 13.

Watu wawili wauawa na 26 kujeruhiwa siku ya Jumamosi, kulingana na vyombo vya habari vya ndani

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, idara ya huduma za dharura zimeripoti vifo viwili wakati wa maandamano ya Jumamosi, pamoja na 26 kujeruhiwa. Waandishi wa habari wa AFP walisikia milio ya risasi wakati wa maandamano hayo. Milio ya risasi na milipuko bado ilisikika katikati mwa mji mkuu baada ya giza kuingia. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na maguruneti kuwatawanya maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu.

Rais Rajoelina “bado yuko Madagascar,” ofisi ya rais inahakikisha

Mwanahabari wetu huko Antananarivo, Sarah Tétaud, anaripoti matukio ya hivi punde ya siku hii yenye matukio mengi nchini. Waziri Mkuu Ruphin Zafisambo, aliyeteuliwa Oktoba 6, ametoa “hotuba fupi ya chini ya dakika nne.” Amehutubia taifa kwa maneno haya: “Serikali imesimama, na niko tayari kuwasikiliza vijana, vyama vya wafanyakazi, na jeshi. Natoa wito kwa askari wenzangu kuepuka kuuana. Tuaminiane, tupendane. Jeshi moja, wananchi wote ni raia wa Madagascar, nchi moja. Madagascar haitavumilia tena mgogoro wowote ikiwa utengano huu wa wananchi utaendelea.” “Amehitimisha kwa kusema kwamba akiwa Waziri Mkuu, alikuwa tayari kuwasiliana na ‘ndugu zake’ huko Capsat kwa manufaa ya watu,” anaongeza Sarah Tétaud.

“Waache waondoke madarakani,” Kanali Mickaël Randrianirina aiambia RFI

Saa 12:15 jioni huko Antananarivo kwenye eneo la Mei 13, Kanali Mickaël Randrianirina, akiwa ndani ya gari la kivita, alihutubia umati wa maelfu ya watu waliokuwa wamekuja kuandamana. Mara baada ya hapo, alijibu maswali kutoka kwa mwandishi wa RFI nchini Madagascar, Sarah Tétaud.

“Tulitoka Capsat kwa ajili ya kuongozana na watu, na wakati tunapita mbele ya Toby ya Ratsimandrava, kulikuwa na gari la kivita la polisi ambalo lilitupiga risasi mara mbili. Waliwapiga risasi askari mmoja na mwandishi wa habari. Mwandishi wa habari alijeruhiwa, na askari huyo alifariki,” aliongeza.

Kisha, Kanali Mickaël Randrianirina akarudia maneno yake aliyozungumza mbele ya umati waandamanaji: “Kama sikuwa Mkristo, ningesema ‘jicho kwa jicho, jino kwa jino.’ Lakini mimi ni Mkristo, kwa hiyo nataka kusema: ‘Kwa wale wote waliotuma maafisa wa polisi hapa, kuanzia mkuu wa polisi, waziri wa polisi, Waziri Mkuu mpya kabisa, na Rais wa Jamhuri: waondoke madarakani.’ Ni hayo tu.”

Na ikiwa Rais Rajoelina atajiuzulu, nani atachukua madaraka na kuongoza nchi? “Tutaangalia,” amesema kanali, ambaye “hajui” kama tukio hilo linaweza kuitwa jaribio la mapinduzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *