
Marais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri na wa Marekani Donald Trump ndio watakaouongoza mkutano huo. Viongozi wengine kutoka zaidi ya nchi 20 wanatarajiwa kuhudhuria na miongoni mwao ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, mwenzake wa Italia Giorgia Meloni na Pedro Sanchez wa Uhispania.
Ufaransa na Uturuki pia kuhudhuria
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Mfalme wa Jordan Abdullah II pamoja na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Antonio Costa atakayeiwakilisha Jumuiya ya Umoja wa Ulaya. Ofisi ya Rais wa Misri imesema lengo la mkutano huo ni kuvimaliza vita katika Ukanda wa Gaza, kuimarisha juhudi za kufikia amani na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati na kuanzisha enzi mpya ya usalama na utulivu wa kikanda.