Shirika la Israel linalosimamia misaada kwa ajili ya Ukanda wa Gaza limesema misaada itakayopelekwa kwenye maeneo ya Wapalestina inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia shehena za malori 600 kwa siku kuanzia leo.

Maandalizi pia yanaendelea kufanyika kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa Gaza na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa nchini Israel. Kwa mujibu wa Gal Hirsch, mratibu wa Israel anayeshughulikia maswala ya mateka na watu waliopotea, watu hao wataachiwa kuanzia Jumatatu.

Juhudi za Trump za kuleta amani Mashariki ya Kati

Wakati huo huo Rais wa Marekani, Donald Trump, aliyesaidia katika juhudi za kuleta amani kati ya Hamas na Israel anatarajiwa kuanza ziara ya Mashariki ya Kati Jumatatu 13.10.2025, ambapo anatazamiwa kulihutubia Bunge la Israel na kukutana na ndugu wa mateka wa Israel na kisha ataelekea nchini Misri ambako ataongoza mkutano wa amani ya Gaza pamoja na Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi. Viongozi wa kikanda na wa kimataifa watahudhuria mkutano huo katika mji wa pwani wa Sharm el Sheikh. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *