
Juhudi za kuwasaidia waliokumbwa na maafa zinaendelea huku serikali ikiwa imewapeleka wanajeshi elfu 10 kwenye eneo lililoathirika.
Kwa mujibu wa taarifa watu wengine 27 bado hawajulikani walipo. Mafuriko na maporomoko ya adhri makubwa yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la kusini mashariki mwa Mexico.
Mamlaka ya Mexico imesema mpaka sasa ni vigumu kuwafikishia maalfu ya watu misaada kwa sababu ni shida kuvifikia vijiji vingi vilivyoathirika na maafa hayo. Wataalamu wa hali ya anga wameonya kuwa mvua zaidi zinatarajiwa kunyesha.