Kiongozi wa upinzani Patrick Herminie ameshinda uchaguzi wa urais nchini Ushelisheli kwa asilimia 52.7 ya kura, Tume ya Uchaguzi ya Ushelisheli imetangaza leo Jumapili, Oktoba 12.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Daktari aliyebobea, Patrick Herminie alikuwa akiwania uongozi kwa tiketi ya chama cha United Seychelles (US), chama kimoja cha zamani ambacho, hadi uchaguzi uliopita, kilikuwa kimewachagua wakuu wote wa nchi tangu mwaka 1977.

“Ushindi wangu ni agizo ambalo watu wameweka ndani yangu,” amesema akionyesha furaha yaka rais wa sita wa Ushelisheli, ambaye ameahidi katika hotuba yake ya ushindi “kupunguza gharama ya maisha na kufufua huduma za umma.”

“Nitakuwa rais wa Washelisheli wote,” ametangaza, wafuasi wake walipokusanyika katika mji mkuu, Victoria, kusherehekea ushindi wake.

Mkuu wa nchi anayemaliza muda wake amekiri kushindwa. “Ninaondoka na urithi ambao unaweza kuwafanya marais wengi kuona haya,” amesema Wavel Ramkalawan. “Natumai Rais Herminie ataendelea kudumisha kiwango hiki,” ameongeza.

Patrick Herminie alishtakiwa kwa “uchawi” mwishoni mwa mwaka 2023. Alielezea mashtaka haya kama “ya kisiasa,” na mashtaka haya yalifutwa miezi michache baadaye. Akiwa daktari, aliongoza shirika la serikali la kupambana na dawa za kulevya.

Rais mpya wa Ushelisheli huenda alinufaika kutokana na rekodi iliyokosolewa ya rais anayemaliza muda wake, kasisi wa Kianglikana, juu ya ulanguzi wa dawa za kulevya-ingawa suala hilo halikutawala mijadala iliyoongoza hadi kupiga kura.

US pia ilishinda uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa mwezi Septemba. Patrick Herminie alimshinda Wavel Ramkalawan, rais aliyeko madarakani na kiongozi wa chama cha Linyon Democratik Seselwa (LDS, Seychelles Democratic Union). Rais huyu anayemaliza muda wake aliongoza upinzani kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2011 na kutoka mwaka 2015 hadi mwaka2020, kabla ya kuchukua mamlaka mwaka huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *