
Zoezi hilo linafanyika katika vituo 31,000 vya kupigia kura kote nchini humo.
Raia wanagapi Cameroon wamejiandikisha kupiga kura?
Raia wasiopungua milioni nane wakiwemo zaidi ya 34,000 wanaoishi ughaibuni wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo.
Biya anayepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi anachuana na wagombea 11. Mpinzani wake mkubwa ni aliyekuwa waziri wa ajira Issa Tchiroma Bakary. Matokeo ya uchaguzi katika nchi hiyo yenye zaidi ya watu milioni 29 yanatazamiwa kutolewa Oktoba 26.