AZAM FC KUANDAA SAFARI YA MASHABIKI: “Azam FC ni burudani na sehemu yenye furaha tu”

AZAM FC KUANDAA SAFARI YA MASHABIKI: “Azam FC ni burudani na sehemu yenye furaha tu”
Katibu wa Mashabiki wa Azam FC, Ahmed Jobenyo, ametoa wito kwa wale mashabiki ambao wanakosa furaha kwenye timu zao, kujiunga na vijana hao wa mitaa ya Chamazi.

Jobenyo amesema wameandaa safari ya mashabiki kutoka bara kwenda Zanzibar kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM.

Katibu huyo wa mashabiki amesema safari itakuwa Jumamosi asubuhi na mechi yao ni saa 10:15 jioni katika dimba la New Amaan Complex.

Azam FC imekuja na ofa kabambe ambapo atakayenunua jezi ‘orijino’ ya timu hiyo, anapewa fulana (T’shirt) bure.

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#Viwanjani #AzamFC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *