AZAM FC YAJA NA OFA KABAMBE: “Ukinunua jezi yoyote ya Azam FC, unapata na fulana kali kabisha bure”
Meneja Masoko na Mauzo wa Azam FC, Ayoub Shelukindo amesema kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya KMKM ya Zanzibar, klabu hiyo kupitia idara yake imepanga kukuza chapa yake kwa kuleta ofa ya kipekee ambapo mtu akinunua jezi, anapata na fulana nyingine bure.
Shelukindo amesema ofa hiyo ni kwa watu wote haijalishi ni shabiki wa timu gani kwasababu Azam FC inakwenda kwenye michuano ya kimataifa.
Azam FC itamenyana na KMKM Oktoba 18, katika dimba la New Amaan Complex.
Shelukindo anasema wanazo jezi hadi za shilingi 9,000 tena orijino na atakayenunua anapata na fulana nyingine bure.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Viwanjani