#HABARI: Mbunge wa viti maalum mstaafu, Felista Njau, ameibukia Tarime mkoani Mara na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ni wajibu wa taifa kuandika historia ya fahari kwa kuwa na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Tanzania.
Akizungumza mbele ya wananchi wa mji wa Tarime, mkoani Mara, Njau amesema Dkt. Samia ameonyesha uthubutu, uongozi wa maono, na moyo wa kujali watu wake katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wake.
“Twendeni tukaandike sura mpya. Kwa mara ya kwanza tumepata mama kwenye nafasi ya urais, hatujawahi kumpata na hatujui itatokea lini tena. Tumuunge mkono, tumlinde, na tumpigie kura ya ushindi,” alisema Njau huku akishangiliwa na wananchi.
Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia, sekta ya afya imeimarika kwa kasi kubwa, ambapo vituo vya afya na huduma za dharura zimeongezeka katika maeneo mbalimbali, hatua iliyookoa maisha ya kina mama na watoto.
“Mama akiwa mzima, familia inatulia. Dkt. Samia alianza na afya ya mama na mtoto, ameongeza vituo vya afya, ameokoa maisha. Huyu ni mama mwenye maono na moyo wa upendo,” alisisitiza Njau.
Mbunge huyo mstaafu amesema pia miradi ya maji imekuwa kipaumbele kikubwa katika serikali ya awamu ya sita, ikiwemo ule wa Tarime unaolenga kufikisha maji safi katika kila kaya.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania