Hamas imewakabidhi mateka hai 20 wa Israeli kwa shirika la Msalaba Mwekundu huko Gaza, leo Oktoba 13, 2025.

Kituo cha habari cha umma cha Israel kimesema kundi hilo liliwaachilia mateka hao kwa awamu mbili, ambapo kundi la pili lenye mateka 13 liliwasilishwa huko Khan Yunis katika Ukanda wa Kusini wa Gaza.

Mabadidhiano haya, yanayofanyika chini ya mpango wa kusitisha mapigano uliofadhiliwa na Marekani, yanaashiria hatua ya kwanza kubwa kuelekea kumaliza vita vya miaka miwili vilivyoiteketeza Gaza na kusababisha maafa makubwa pande zote mbili.

Mapema Jumatatu, Hamas ilitoa orodha ya mateka 20 walio hai watakaoachiliwa, pamoja na orodha ya zaidi ya wafungwa 1,900 wa Kipalestina wanaotarajiwa kuachiwa na Israel.

Jeshi la Israel limesema mateka hao wataanza kukabidhiwa kwa maafisa wa Msalaba Mwekundu kabla ya kupelekwa katika vituo vya kijeshi kwa uchunguzi wa afya na kuunganishwa na familia zao.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *