
Shirika la habari la umma la Israel limeripoti kwamba, kundi la Hamas limekabidhi hivi leo Jumatatu, mateka 20 walio hai wa Israel kwa wawakilishi wa shirika la msalaba mwekundu katika Ukanda wa Gaza.
Mateka hao wamekabidhiwa katika makundi mawili na kusafirishwa katika mji wa Khan Yunis Kusini mwa Ukanda wa Gaza kama sehemu ya makubaliano ya usitishaji vita ambayo wengi wanatarajia yataashiria mwisho wa vita vya miaka miwili vilivyoliharibu kabisa eneo zima la Ukanda wa Gaza.
Miongoni mwa mateka hao ni wanajeshi na raia baadhi yao walitekwa katika tamasha la muziki la Nova ambako takriban watu 400 waliuwawa.