IRAN vs TANZANIA: “Inaweza kutumika kama sehemu ya kujenga wachezaji wadogo”
Mchambuzi wa soka nchini Jemedari Said Kazumari amesema mechi ya kesho ya kirafiki kati ya Irani dhidi ya Tanzania, ni nafasi kwa vijana wapya ambapo itawasaidia kukuza ufahamu wao kwenye maswala ya mbinu.
Jemedari amesema mechi hizi za kirafiki zitasaidia kwa wachezaji wadogo kuendelea kukuza uzoefu kuelekea michuano ya AFCON 2025 na 20227.
Wachambuzi wengine waliozungumza ni pamoja na Juma Ayo, Godlisten Muro, Ibrahim Kasuga na Hussein Bakari.
Mechi hiyo ya kirafiki itapigwa saa 12:00 jioni na itakuwa LIVE #AzamSports1HD
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#TaifaStars