Umoja wa Ulaya umeeleza kuwa usitishaji vita huko Gaza ni fursa ya kweli ya kuhitimisha vita vya uharibifu.

Umoja wa Ulaya umekaribisha na kuunga mkono makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza, na kusema kuwa makubaliano hayo ni fursa ya kweli ya kumaliza vita vya uharibifu na mateso ya watu wa eneo hilo. Mwakilishi wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kupitia taarifa aliyoitoa kwamba: Umoja wa Ulaya unakaribisha makubaliano ya awamu ya kwanza ya mpango wa kina wa kumaliza vita huko Gaza uliowasilishwa na Rais wa Marekani Donald Trump ili kuhakikisha vita vinasimamishwa na matela wote wanaachiwa huru haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya Umoja wa Ulaya imeongeza kuwa: Tunatoa wito kwa pande zote kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo bila kuchelewa na kufanikisha usitishaji vita wa kudumu, kuwaachia huru mateka, kuruhusu uingizaji na usambazaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu huko Gaza bila  bila vizuizi au ukwamishaji wowote.

Umoja wa Ulaya umesisitiza kuwa: Fursa hii ya kweli iliyopatikana ni kwa ajili ya kuhitimisha vita vya uharibifu, mateso na kuandaa njia moja ya kisiasa kwa usalama na amani ya kudumu kuelekea suluhisho la serikali mbili. Taasisi hiyo ya Ulaya imeongeza kusema: Umoja wa Ulaya uko tayari kustafidi na wenzo mbalimbali  ili kufanikisha utekelezaji wa mpango wa kina wa kuhitimisha vita katika Ukanda wa Gaza. 

Mtazamo jumla:

Inaonekana kuwa, Umoja wa Ulaya umechukua msimamo jumla na wa tahadhari mkabala wa mpango wa amani wa Donald Trump wa nukta 20 kwa ajili ya Gaza. Mpango huo unaojumuisha suala la kusitisha vita haraka iwezekanavyo, kuwaachia huru mateka, ujenzi mpya wa Gaza na kuasisiwa utawala wa muda chni ya usimamizi wa kimataifa umeungwa mkono pakubwa na baadhi ya nchi za Ulaya hata hivyo kuna wasiwasi kuhusu namna utakavyotekelezwa na taathira za muda mrefu za mpango huo. 

Uungaji mkono wa kimsingi:

Wakuu wa nchi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza yaani Emmanuel Macron, Friedrich Mertz na Keir Starmer wameunga mkono mpango huo wa Trump na kuutaja kuwa hatua nzuri kuelekea kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza. Viongozi hao wamesisitiza kuhusu umuhimu wa kuwaacha huru mateka, kuruhusu tena misaada ya kibinadamu kuingiza Gaza na wakat huo huo wamepogeza  nafasi yawapatanishi wa kikanda kama Misri, Qatar na Uturuki. 

Wasiwasi na ukosoaji: 

Pamoja na haya yote, baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya wameeleza wasiwasi wao kuhusu mpango huo wa Trump utakavyotekelezwa. Viongozi hao hasa wamekosoa kukosekana  ratiba inayoeleweka kuhusu utekelezaji wa mpango huo wa Trump, kuwepo sintofahamu kuhusu nafasi ya baadaye ya Hamas huko Gaza, na kutoashiriwa njia ya ufumbuzi wa serikali mbili.

Nafasi ya Umoja wa Ulaya katika awamu ya kwanza ya utekelezaji:

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa uko tayari kushiriki katika marhala ya utekelezajiwa mpango wa Trump. ushiriki huo unajumuisha uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu, kusaidia kufanyika marekebisho ndani ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kusimamia kivuko cha Rafah na kushiriki katika kuijenga upya Gaza. Kaja Kallas Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa umoja huo uko tayari kushirikiana na washirika wake wa kikanda na kimataifa ili kutekeleza mpango huu tajwa. 

Kaja Kallas

Dira: 

Umoja wa Ulaya pia unaendelea kutilia mkazo juu ya haja ya kupatikana njia ya ufumbuzi wa serikali mbili, na unaamini kuwa hiyo ni njia pekee ya utatuzi wa kudumu kwa ajili ya amani katika kanda hii. Kuhusiana na hili, Umoja wa Ulaya umebainisha kuwa uko tayari kuiunga mkono Mamlaka ya ndani ya Palestina katika kutekeleza mageuzi na kuijenga upya Gaza. Kijumla, Umoja wa Ulaya pamoja na kuunga mkono kwa tahadhari mpango huo wa Trump umesisitiza kuwa unaunga mkono kutekelezwa kwa umakini na kwa uwazi mpango huo na kusema ukko tayari kushiriki kuutekeleza mpango huo. 

Tarehe 29 mwezi Septemba mwaka huu akiwa pamoja na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel mbele ya waandishi wa habari, Trump alizindua mpango wenye nukta 20 kwa ajili ya kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza. Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) pia Oktoba 3 ilitoa jibu mkabala wa mpango huo wa Trump na kutangaza kuwa  inaafikia suala la kusitisha kikamilifu vita huko Gaza, kubadilishana mateka na Gaza kujiendeshea masuala yake na kutaka kuchunguzwa mustakbali wa Gaza katika fremu ya maslahi ya taifa la Palestina. Nalo jeshi la utawala wa Kizayuni Ijumaa adhuhuri likatangaza rasmi kwamba usitishaji vita umeanza kutekelezwa katika Ukanda wa Gaza. 

Wakat huo huo televisheni ya al Jazira yenye makao yake Qatar Ijumaa usiku ilitangaza kuwa imepata waraka kuhusu marhala za utekelezaji wa mpango wa Trump kwa ajili ya kuhitimisha vita katika Ukanda wa Gaza; ambapo kwa mujibu wa waraka khuo, vita  vitasimamishwa Gaza ndani ya saa 72 baada utawala wa Kizayuni na Hamas kufikia makubaliano.  Kwa mujibu wa vipengee vya mpango huo, misaada ya kibinadamu ilipasa kuingia Ukanda wa Gaza mara tu baada ya kutangazwa makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *