Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mary Maganga, amewataka vijana kote nchini kutumia haki yao ya kuchagua viongozi wanaoakisi matumaini na malengo ya taifa.

Akizungumza katika Kongamano la Vijana Tanzania jijini Mbeya, amesema vijana ni nguvu ya mabadiliko, hivyo wanapaswa kuchagua viongozi wenye dira sahihi kwa maendeleo ya taifa.

Ameeleza kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mikakati ya kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii, ikiwemo utoaji wa mikopo na fursa za ajira.

Kongamano hilo limewakutanisha zaidi ya vijana 1,500 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *