KUTOKA DUBAI: Msafara wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) hii leo umealikwa katika ofisi za ubalozi mdogo wa Tanzania katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa Dubai.
Msafara huo wa Stars ukiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman Ali (Morocco) umepokewa na maofisa ubalozi na Balozi mwenyewe Luten Jenerali mstaafu Yacoub Mohammed.
Taifa Stars ipo Dubai kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Iran. Mechi hiyo itapigwa kesho Jumanne saa 12:00 jioni na itakuwa LIVE #AzamSports1HD
Wenzetu Chrispin Hauli na Shishira Mzava wapo kwenye msafara huo.
#TaifaStars