Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua serikali mpya Jumapili baada ya mazungumzo marefu ya kuunda baraza jipya la mawaziri ili kuepusha taifa hilo kuingia katika mgogoro wa kisiasa.

Waziri Mkuu Sebastien Lecornu ameunda serikali yake ya pili, yenye mchanganyiko wa sura mpya na za zamani, akilenga kupitisha bajeti ya kubana matumizi katika bunge lililogawanyika.

Jean-Noel Barrot asalia kwenye wadhifa wake

Kulingana na orodha iliyotolewa na Ikulu ya Élysée, Jean-Noël Barrot amebaki kama waziri wa mambo ya nje, Catherine Vautrin amechukua wizara ya ulinzi, huku Roland Lescure akisimamia uchumi.

Laurent Nunez ameteuliwa waziri wa mambo ya ndani, na Monique Barbut kuchukua wizara ya mazingira.

Lecornu anakabiliwa na changamoto kubwa ya kisiasa, kwani vyama vya upinzani vimeapa kupinga serikali yake, huku Rais Macron akikabiliwa na shinikizo jipya kabla ya safari yake kuelekea Misri kujadili makubaliano ya kusitisha vita Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *