Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Agnesta Lambert Kaiza amewataka vijana kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kutosusia uchaguzi.
Agnesta, amesena kupiga kura ni haki ya kidemokrasia na endapo hawatojitokeza watapoteza hakli hiyo.
“Ni wasihi vijana wote wa Jimbo la Segerea kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 29 na asibaki yoyote nyumbani ili kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindi. Msikubali kuchaguliwa vingozi wenu na watu wachache,” ameongeza Agnesta.
Mgombea huyo amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 13,2025 akizungumza katika kipindi cha Bonanza kinachorushwa na Radio Free Africa.
#StarTvUpdate