Mgombea ubunge wa jimbo la Chaani, Ayoub Mohamed Mahmoud na mgombea uwakilishi wa jimbo hilo Juma Usonge Hamad wameahidi kuongeza kasi ya maendeleo pamoja na upatikanaji wa huduma bora za kijamii iwapo watachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.

Sambamba na hayo wawili hao pia wameahidi kuongeza chachu ya upatikanaji wa ajira kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanyika katika jimbo hilo.

Wameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi zilizofanyika Kinyasini mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mhariri @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *