Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake katika miaka mitano ijayo, itauboresha Uwanja wa Ndege wa Chato na kujenga mpya Geita Mjini, mkoani Geita.
Sambamba na hayo, amesema katika kipindi hicho, ataiboresha pia Hifadhi ya Wanyamapori ya Burigi wilayani Chato, katika Mkoa wa Geita ili kuinua sekta ya utalii mkoani humo.
Dkt Samia ametoa ahadi hizo leo, Jumatatu Oktoba 13, 2025 alipozungumza na wananchi wa Geita Mjini, katika mkutano wake wa kampeni za urais, zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Amesema Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2025/30 inaielekeza Serikali kuendeleza Uwanja wa Ndege Chato na kujengwa Uwanja wa Ndege Geita Mjini, ili kurahisisha usafiri wa anga.
Katika sekta ya maliasili na utalii, amesema ilani hiyo inaelekeza kuboreshwa kwa Hifadhi ya Bugiri Chato mkoani humo na udhibiti wa wanyama waharibifu utaendelea kufanyika.
#StarTvUpdate