Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (XCCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema alifundishwa na kulelewa vema na Rais wa…Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (XCCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema alifundishwa na kulelewa vema na Rais wa…

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (XCCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema alifundishwa na kulelewa vema na Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli, ndio maana amefanikiwa kukamilisha miradi iliyoanzishwa na mtangulizi wake huyo.

Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 baada ya kuugua maradhi ya umeme wa moyo. Machi 19, Dkt Samia aliapishwa kuwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Oktoba 13, 2025 alipozungumza na wananchi wa Chato mkoani Geita, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

“Mimi najazia, alikuwa ni mwalimu mzuri na mlezi mahiri. Ndiyo maana kazi tuliyoianza awamu ya tano, nimeweza kwenda nayo vizuri kwa sababu alinielekeza vizuri na alinilea vema ndio maana nimeweza,” amesema.

Amesema hayati Magufuli alifariki akiwa ameliacha Bwawa la Umeme la Julius Nyerere likiwa asilimia 37, lakini sasa amelikamilisha na umeme unazalishwa.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *