MSIGWA AFAFANUA KUHUSU DIMBA LA MKAPA: “Ule uwanja ni wa nyasi halisi, nyasi halisi zina utaratibu wake wa matumizi”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, ametoa wito kwa Watanzania kuacha kuuita majina ya kebehi Uwanja wa Benjamin Mkapa akisema kwamba viwanja vyenye nyasi asilia huwa kuna utaratibu maalumu wa kutumika.
Msigwa amesema utaratibu wa viwanja vyenye nyasi asilia, ni kwamba kila baada ya miaka mitatu, inatakiwa kubadilishwa tabaka lote la juu na kuwekwa tabaka lingine ambapo katika dimba la Benjamin Mkapa, jambo hilo lilifanyika mara ya mwisho mwaka 2019
Msigwa amesema kwa sasa wameanza mchakato wa kumtafuta mkandarasi ili kubadilisha tabaka la juu la uwanja na kuwekwa tabaka jipya.
Msigwa amesema wametafuta ‘dawa’ ya wale wenye tabia ya kufanya uharibifu wa miundombinu katika dimba la Benjamin Mkapa.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Viwanjani #Msigwa