MSIGWA AIZUNGUMZIA CHAN 2024, AFCON 2027: “CHAN peke yake sisi serikali, imetugharimu shilingi bilioni 45 kuboresha miundombinu ...

MSIGWA AIZUNGUMZIA CHAN 2024, AFCON 2027: “CHAN peke yake sisi serikali, imetugharimu shilingi bilioni 45 kuboresha miundombinu yetu”

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, ametoa wito kwa taasisi binafsi kutumia vema fursa zitokanazo na michuano mbalimbali ya soka inayofanyika nchini.

Msigwa amesema serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kuandaa michuano ya CHAN 2024 na itatoa pia kwenye kuandaa michuano ya AFCON 2027.

Kwasababu hiyo basi, Watanzania kutoka sekta mbalimbali wanapaswa kuzichungulia fursa ili waweze kunufaika na michuano hiyo.

Msigwa pia amesema kwa kuandaa michuano ya CHAN 2024, serikali imejifunza namna bora ya kufanya maandalizi hasa kuelekea AFCON 2027.

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#Viwanjani #Msigwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *