MSIGWA ASEMA SPORTS ARENA INAKUJA: “Tutajenga kijiji ama mji wa filamu pale Kwala Pwani”

MSIGWA ASEMA SPORTS ARENA INAKUJA: “Tutajenga kijiji ama mji wa filamu pale Kwala Pwani”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali amesema Rais Samia Suluhu Hassan anawekeza katika michezo na burudani, kwasababu anaamini huko nako kuna fursa nyingi na ni eneo ambalo linachangia kwenye uchumi.

Msigwa amesema kwa kuliona hilo, ndio maana upo mpango wa kujenga ukumbi wa burudani na michezo (Sports arena) na mji wa filamu.

Msigwa amesema katika ule utaratibu wa fedha za goli la Mama, ni kwamba timu hata ishinde magoli mangapi, fedha za kupewa zitakuwepo na hakuna utaratibu wa kusema kwamba itatokea siku hela zitakuwa chache na kumlazimu arudi mbio kuzifuata.

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#Viwanjani #Msigwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *