Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ezekiah Wenje, amesema si Serikali iliyokizuia chama hicho cha upinzani kushiriki uchag…Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ezekiah Wenje, amesema si Serikali iliyokizuia chama hicho cha upinzani kushiriki uchag…

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria, Ezekiah Wenje, amesema si Serikali iliyokizuia chama hicho cha upinzani kushiriki uchaguzi, bali kiliamua chenyewe.

Wenje ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Oktoba 13, 2025 alipotangaza uamuzi wa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika Chato mkoani Geita

Katika hotuba yake hiyo, Wenje ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, amesema ni uzushi kwa chama hicho cha upinzani kudai kimezuiwa na Serikali kushiriki uchaguzi, kwani chenyewe kupitia vikao vyake, kilikaa na kuamua kusishiriki.

“Januari 20 mwaka huu, tulikuwa Dar es Salaam tukafanya kitu kinachoitwa Baraza Kuu la chama, likatoa mapendekezo, tukapeleka kwenye mkutano mkuu wa chama, sote tukakubaliana kwamba Chadema hatushiriki uchaguzi.

“Sasa nani amekukatalia kushiriki uchaguzi, sisi tuliamua kuweka mpira kwapani tumeogopa tukaenda,” amesema.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *