Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, amesema maandamano pekee ambayo vijana na wananchi wanapaswa kufanya ni kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao, ili kuendeleza kasi ya maendeleo inayoletwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa matembezi ya kumkaribisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Magambo alisema vijana wa Geita na Watanzania kwa ujumla wamefunguka kisiasa na wanajua kuwa sauti yao halisi ni kura, si vurugu wala maandamano barabarani.
Aliongeza kuwa vijana wa UVCCM wanatambua mchango mkubwa wa Rais Samia katika kuinua uchumi wa vijana kupitia miradi ya maendeleo, mikopo, na fursa za ajira, hivyo wana kila sababu ya kumuunga mkono kwa vitendo.
#starTvUpsate