cx

Chanzo cha picha, Getty

Kylian Mbappe amefunga mabao 17 katika mechi 13 akiwa na Real Madrid na Ufaransa msimu huu.

Harry Kane, 32, amefunga mabao 19 katika mechi 12 akiwa na Bayern Munich na England.

Na Erling Haaland, 25, anaongoza kwa mabao 21 katika michezo 12 kwa Manchester City na Norway.

Watatu hao kwa sasa wako katika kiwango kizuri kuliko washindani wao wengine.

Mfano, Ousmane Dembele wa Paris St-Germain, ambaye alishinda Ballon d’Or hivi karibuni, amecheza mara tano pekee msimu huu kwa sababu ya majeraha.

Pia unaweza kusoma

Kuwalinganisha wachezaji watatu

Haaland ndiye aliyefunga mabao mengi zaidi kati ya hao watatu msimu huu huku mabao yake 21 katika mechi 12 yakiwa ni wastani wa moja kila baada ya dakika 47.

Kane jumla ya mabao 19 kati ya mechi 12 ni sawa na goli moja kila dakika 52, na Mbappe ana wastani wa kufunga moja kila dakika 67 na mabao yake 17 katika mechi 13.

Mbappe ana pasi nne za mabao, huku wengine wawili wakiwa wametoa pasi tatu kila mmoja.

Mbappe amegusa mpira mara 772, zaidi ya Kane mara 445 na Haaland mara 257.

Haaland ametengeneza nafasi sita pekee kwa wachezaji wenzake, ikilinganishwa na nafasi 38 za Mbappe na Kane 27.

Na ukulinganisha idadi ya pasi kamili kwa kila fowadi – pasi 97 za Haaland, 456 za Mbappe na 231 za Kane.

Raia huyo wa Norway amechukua mipira kutoka juu mara 25 – huku 12 kwa Kane na tatu kwa Mbappe.

Kane ndiye mfungaji mabao hatari zaidi kati ya hao tatu msimu huu huku 42% ya mashuti yake 45 yakisababisha bao, akifuatiwa kwa karibu na 39% ya mashuti 54 ya Haaland – huku Mbappe akifunga 22% ya mashuti yake 77.

Kane katika msimu huu ameifungia Uingereza goli moja tu, huku Haaland akiifungia Norway mabao tisa naye Mbappe akiifungia Ufaransa mara tatu.

Mataifa yote matatu ni vinara wa makundi yao ya kufuzu Kombe la Dunia.

Kane

vc

Chanzo cha picha, Getty

Mfungaji bora wa England, Kane amefikisha mabao 18 kwa Bayern katika mechi 10 msimu huu, ikijumuisha 11 kwenye Bundesliga na manne kwenye Ligi ya Mabingwa – pamoja na bao moja kwa nchi yake.

Amefunga 47% ya mabao 38 ya Bayern msimu huu. Amefunga mabao matatu matatu dhidi ya Leipzig na Hoffenheim.

Ikiwa Kane ataweza kuendelea na kiwango hiki cha mabao katika Bundesliga msimu mzima, atamaliza akiwa na mabao 62. Hakuna aliyewahi kufunga mabao mengi kiasi hicho katika ligi kuu ya Ulaya.

Rekodi ya Bundesliga ni mabao 41 ambayo Lewandowski aliifungia Bayern msimu wa 2020-21.

Mfungaji bora wa muda wote wa Tottenham ameshinda Kiatu cha Dhahabu katika misimu miwili akiwa na Bayern, akiwa na mabao 36 na kisha mabao 26, na kuongeza kwenye tuzo zake tatu za Ligi Kuu ya Uingereza.

Ikiwa atakuwa mfungaji bora msimu huu pia, kutamfanya kuwa mtu wa pili kushinda mfugaji bora mara tatu mfululizo kwenye Bundesliga baada ya Lewandowski (aliyeshinda mara tano mfululizo).

Mbappe

fdc

Chanzo cha picha, Getty

Mbappe amefunga mara 14 katika mechi 10 za Real msimu huu – na mabao matatu kati ya mechi tatu akiwa na Ufaransa.

Hiyo ni 54% ya mabao 28 ya Real Madridi katika mashindano yote. Ni dhidi ya Mallorca pekee ambapo ameshindwa kufunga – na amefunga magoli matatu katika mechi moja kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kairat Almaty.

Ikiwa Mbappe ataendelea na kiwango chake cha kufunga mabao tisa katika mechi nane kwenye La Liga, atakuwa na mabao 42.

Ni Lionel Messi pekee (mara mbili) na Cristiano Ronaldo ndio wana magoli mengi katika msimu katika ligi kuu ya Uhispania.

Anawinda Kiatu cha Dhahabu cha nane mfululizo baada ya kushinda sita mfululizo kwenye Ligue 1 akiwa na PSG (yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote) na ni mfungaji bora mwaka jana wa La Liga huko Real.

Katika Ligi ya Mabingwa, amefunga mabao matano katika mechi mbili.

Kiwango hicho cha mabao kinampa nafasi ya kuwinda rekodi ya Ronaldo ya kufunga mabao 17 katika msimu wa Ligi ya Mabingwa (2013-14).

Pia atatumaini kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ufaransa msimu huu utakapomalizika. Amefunga mabao 53, manne pekee nyuma ya rekodi ya Olivier Giroud.

Haaland

fd

Chanzo cha picha, Getty

Ni mfungaji bora wa muda wote wa Norway amefunga mabao 12 katika mechi tisa alizoichezea City. Mechi dhidi ya Tottenham ndio timu pekee iliyomkosesha bao.

Lakini akiwa na Norway ameshinda magoli tisa katika mechi tatu (ikiwa ni pamoja na matano dhidi ya Moldova na matatu dhidi ya Israel) na kuwapeleka ukingoni mwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1998, kabla ya kuzaliwa kwake.

Amefunga mara 12 wakati wa mechi za kufuzu Kombe la Dunia hadi sasa, mara mbili zaidi ya mchezaji yeyote wa Ulaya.

Haaland ameweka rekodi kubwa ya mabao tisa katika michezo saba ya kwanza ya Ligi Kuu ya msimu huu, ni rekodi ya tatu kwa ubora katika hatua hii katika misimu yake minne nchini Uingereza.

Alikuwa ametikisa nyavu mara 11 kufikia sasa 2022 na mara 10 msimu uliopita.

Ikiwa atakwenda na kiwango chake cha sasa cha kufunga kwenye ligi kitamletea mabao 49. Rekodi yake kubwa ya Premier League ni 36 alipofunga 2022-23.

Ikiwa tu tutahesabu takwimu zake za City msimu huu, yuko mbioni kufunga takriban mabao 70 vilabu katika mashindano yote ikiwa watatinga fainali ya Ligi ya Mabingwa (bila yeye hata kucheza Kombe la Carabao au Kombe la FA).

Ukituruhusu kujumuisha jumla cha mabao kwa klabu na nchi, anaweza kumaliza msimu kwa zaidi ya mabao 100.

Nani nani bora zaidi?

Winga wa zamani wa Scotland, Chelsea na Everton Pat Nevin, na mchambuzi wa BBC Sport, anasema: “Siyo kumdharau Erling Haaland, ambaye ni mmoja wa wachezaji wakubwa katika soka la dunia. Lakini nchini Uingereza, Harry ndio huonekana bora.”

Mwandishi wa habari wa soka wa Uhispania Guillem Balague, anafikiri Mbappe na winga wa Barcelona Lamine Yamal ndio wachezaji wawili bora wa nafasi yoyote duniani hivi sasa.

Wakati mchezaji mwenzake wa Manchester City Nico Gonzalez anaamini Haaland ndiye “mshambulizi bora zaidi duniani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *