Photos from AzamSports's post

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amefanya ziara ya kukagua dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, ambaopo kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo ni kwamba ukarabati wake umefikia asilimia 90.

Taarifa ya Wizara inaeleza kuwa Msigwa amefanya ziara hiyo leo Oktoba 13, 2025 akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wake Methusela Ntonda .

Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni pamoja na ufungaji wa taa mpya za kisasa, uwekaji wa nyasi bora za bandia (Pitch), marekebisho ya njia za kukimbilia (Running Track), ufungaji wa viti vipya, ukarabati wa vyoo, ufungaji wa milango mipya na uwekaji wa vigae vipya pembezoni mwa uwanja.

#Uhuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *