Rais wa Marekani, Donald Trump, amewasili nchini Israel kupitia Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion, ambapo amepokelewa na Rais wa Israel, Isaac Herzog, pamoja na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Trump amewasili kwa ndege ya rais wa Marekani, Air Force One, huku tukio hilo likiambatana na furaha ya kurejeshwa kwa kundi la kwanza la mateka kutoka Ukanda wa Gaza waliokuwa wametekwa kwa takriban miaka miwili.
Mapokezi hayo ya hadhi ya juu yameonesha mshikamano wa karibu kati ya Israel na Marekani, hasa katika kipindi ambacho Ukanda wa Gaza na eneo lote la Mashariki ya Kati linaendelea kukumbwa na mvutano wa mara kwa mara.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mblamwezi