Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege ya Dodoma imekabidhiwa kisima cha maji safi na salama na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa miaka miwili iliyopita na mamlaka hiyo.

Kisima hicho chenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 20 kinatarajiwa kutatua changamoto ya maji kwa wanafunzi, walimu na wakazi wa maeneo ya karibu na shule hiyo.

Kisima hicho kimekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCAA, Dkt. Hamis Mwinyimvua aliyeahidi mamlaka hiyo kuendelea kuwa mlezi wa shule hiyo na itaendelea kutatua changamoto za shule hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa wajibu wake wa kurudisha kwa jamii.

“Maji ni uhai, na tunataka kila mwanafunzi hapa ajifunze katika mazingira safi na salama na TCAA itabaki kuwa mlezi wa shule hii. Tutazidi kushirikiana na uongozi wa shule kutatua changamoto mbalimbali taratibu, ili kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia yanadumu” alisema Dkt. Mwinyimvua.

Kisima hicho kimekabidhiwa katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya shule hiyo sambamba na mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba.

Mhariri @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *