Wakati huohuo, watu wameingia katika medani kubwa karibu na baraza la jiji la Antananarivo, wakipeperusha bendera, huku wakisubiri hotuba hiyo.

Maandamano hayo yaliyoanza Septemba kwanza yaliangazia kukatika kwa umeme na uhaba wa maji katika nchi hiyo na baadaye yakaendelea na kuwa harakati dhidi ya serikali wakitaka Rajoelina mwenye umri wa miaka 51 ajiuzulu.

Umoja wa Mataifa inasema watu wasiopungua 22 wameuawa katika siku za kwanza, na pia wahalifu wamepora mali.

Rajoelina amekanusha idadi hiyo, akisema wiki iliyopita “vifo 12 vilithibitishwa vya waporaji na waharibifu”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *