.

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona haitamuongezea mkataba mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 37, mkataba wake utakapokamilika msimu ujao. (Sport – In Spanish)

Barcelona wako tayari kuchukua chaguo la kufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji Marcus Rashford, 27 kutoka Manchester United kuwa wa kudumu kufuatia kiwango kizuri cha mchezo wake mapema msimu huu. (Sun)

Kipa wa England Jordan Pickford, 31 anatazamiwa kuongeza muda wake wa kuitumikia Everton kwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na The Toffees. (Times Subscription Required}

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anapanga kurejea kwenye uongozi na angependa kuinoa timu ya Ufaransa. (Mirror)

Newcastle United watafikiria kumruhusu fowadi wa Denmark William Osula, 22, kuondoka kwa mkopo Januari – lakini tu ikiwa chaguzi zao zingine zote zinafaa. (Football Insider)

Arsenal wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Sevilla Lucien Agoume, 23, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Fichajes – In Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wana nia ya kumsajili beki wa Barcelona Ronald Araujo, 26, lakini hawana uwezekano wa kumnunua katika dirisha la Januari. (Football Insider)

Tottenham Hotspur, Liverpool na Aston Villa ni miongoni mwa timu nyingi za Premier League zilizotuma maskauti kumtazama beki wa kati wa FC Nantes Tylel Tati, 17. (CaughtOffside).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *