Rais Donald Trump wa Marekani amewaambia wabunge wa Israel kwamba nchi yao haina cha kukipigania tena katika Ukanda wa Gaza na kwamba nchi hiyo inapaswa kuchukua hatua kuelekea amani katika eneo la Mashariki ya kati, baada ya miaka miwili ya vita dhidi ya kundi la Hamas, Hezbollah na Iran.

Trump ameipongeza Israel kwa kile alichokiita ushindi dhidi ya magaidi kwenye eneo hilo.

”Ushindi na mafanikio ya Israel  tangu October  7 yanapaswa kuuthibitishia ulimwengu kwamba wale wanaotaka kuliangamiza taifa hili wataishia kushindwa vibaya. Taifa la Israel ni imara na litadumu na kuendelea daima”

 Trump pia ameahidi kusaidia ujenzi wa Gaza ambako kumeharibiwa vibaya na vita na mashambulizi ya Israel na kuwatolea mwito kuondoka katika kile alichokiita njia ya ugaidi na vurugu.

Kadhalika ameitumia hotuba yake katika bunge la Knesset kumuomba rais wa Israel kumpa msamaha waziri mkuu Benjamin Netanyahu ambaye anaandamwa na kesi za rushwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *