Rais wa Marekani Donald Trump amewasili nchini Israel Jumatatu, ambako atakutana na familia za mateka na kuhutubia wabunge katika Knesset kabla ya kuelekea Sharm el-Sheikh, Misri, kwa mkutano wa kimataifa kuhusu vita vya Gaza.

Trump alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, muda mfupi baada ya mateka saba waliokuwa wakishikiliwa na Hamas kukabidhiwa kwa jeshi la Israel kupitia shirika la Msalaba Mwekundu. Hamas imesema mateka wote 20 waliokuwa hai wataachiwa leo kwa kubadilishana na wafungwa zaidi ya 1,900 wa Kipalestina.

Israel Tel Aviv 2025 | Donald Trump amsalimia Benjamin Netanyahu katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion
Rais Donald Trump akimsalimia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben Gurion, Jumatatu, Oktoba 13, 2025, karibu na Tel Aviv.Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Trump atamba: ‘Vita vimekwisha’

Akiwa safarini kwa ndege ya Air Force One, Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba “vita kati ya Israel na Hamas vimekwisha.” Baadaye Jumatatu, Trump na Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sissi wataongoza mkutano wa kilele unaolenga kudumisha usitishaji mapigano na kujenga misingi ya amani ya kudumu.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Misri, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria ni Emmanuel Macron wa Ufaransa, Friedrich Merz wa Ujerumani, Keir Starmer wa Uingereza, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *