
Chanzo cha picha, Getty Images
Hamas
inatazamiwa kuwaachilia mateka 48 waliosalia Gaza ifikapo saa sita
mchana (09:00 GMT). Kati ya hao, 20 wanaaminika kuwa hai, na wanatarajiwa
kupelekwa haraka kwa matibabu kabla ya kuunganishwa tena na wapendwa wao. Miili
ya wengine 28 inastahili kurejeshwa.
Haya
yanajiri wakati Rais wa Marekani Donald Trump anafanya ziara nchini Israel kufuatia
makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani, Misri na Qatar.
Trump atalihutubia
bunge la Israel kabla ya kusafiri hadi mji wa wa Misri wa Sharm El-Sheikh
kuandaa mkutano wa kilele wa amani katika Mashariki ya Kati, utakaojumuisha
takriban viongozi wengine 20 wa dunia.
Trump
atapokelewa na “makundi ya Waisraeli kwa shukrani na urafiki”, Rais
wa Israel Isaac Herzog alisema Jumapili, huku Waisraeli wengi wakimsifu rais wa
Marekani kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kwa
mabadilishano ya kurejesha mateka hao, Israel itawaachia huru wafungwa 250
wa Kipalestina, wakiwemo wanaotumikia kifungo cha maisha jela. Hiyo ni pamoja
na kuwaachilia zaidi ya wafungwa 1,700 waliokuwa wakizuiliwa bila kufunguliwa
mashtaka katika kipindi cha vita – wakiwemo karibu Watoto zaidi ya kumi.
Kwingineko, malori
yaliyobeba misaada yanavuka mpaka na kuingia Gaza huku Wapalestina,
waliohamishwa kwa nguvu kuelekea kusini kutokana na mashambulizi ya Israel,
wakiendelea kurejea eneo la kaskazini mwa eneo hilo. Wanakumbana na uharibifu uliotokea,
maeneo makubwa ya Jiji la Gaza yakiwa vifusi.
Soma zaidi: