Wakati ukuaji wa sekta ya madini ukifikia asilimia 4.8 mwaka huu, Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Sam…Wakati ukuaji wa sekta ya madini ukifikia asilimia 4.8 mwaka huu, Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Sam…

Wakati ukuaji wa sekta ya madini ukifikia asilimia 4.8 mwaka huu, Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema dhamira yake ni kuikuza sekta hiyo kwa asilimia tisa mwaka 2030.

Dkt Samia ameeleza dhamira hiyo leo, Jumatatu Oktoba 13, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika Geita Mjini, mkoani Geita.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Serikali yake inalenga kuikuza sekta ya madini kutoa asilimia 4.8 za sasa, hadi kufikia asilimia tisa.

Utekelezwaji wa hilo, amesema utatanguliwa na kuandaa utaratibu wa kutoa mitaji kwa wachimbaji wadogo kuwakuza ili wawe wakubwa, huku maeneo mapya ya uchimbaji yakitafutwa kupitia tafiti.

Pia, amesema katika mkoa huo utajengwa Uwanja wa Maonyesho na Mikutano ya Sekta ya Madini.

#StarTvupdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *