WAKULIMA HABARI:Katika kuhakikisha kuwa zao la kahawa aina ya Arabika kutoka Nyanda za juu Kusini linaendelea kufanya vizuri kwenye soko la kimataifa, wakulima wa kahawa wilayani Mbozi mkoani Songwe, wameanza kunufaika na mafunzo ya kitaalamu pamoja na miche ya miti ya matunda na kivuli, hatua hii inalenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha ustahimilivu wa zao hilo.
Mafunzo hayo yametolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Solidaridad kwa kushirikiana na serikali , ambapo wakulima wamefundishwa mbinu za kilimo mseto za kuchanganya zao la kahawa na mazao mengine rafiki kwa mazingira, ambapo wakulima wakulima wamesema mbinu hizo zitaleta mabadiliko chanya kwenye mashamba yao.
Msimamizi wa mradi huo kutoka solidaridad, bi roselaida ngowi, pamoja na meneja wa Kituo cha Utafiti wa Kahawa (TACRI) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Dismas Pangalas, wamesema kuwa lengo ni kuongeza ubora na uzalishaji wa kahawa huku wakulima wakinufaika kiuchumi na mazingira yakihifadhiwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Mifugo, Uvuvi na kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Bw. George Nipwapwacha, amewapongeza wakulima kwa ushiriki wao na kuwasihi kutumia vyema elimu waliyopewa, ili kuboresha maisha yao na kuongeza ushindani wa kahawa ya Tanzania duniani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania