Watumishi wa idara ya afya katika hospitali za halmashauri mkoani Simiyu wamehimizwa kushiriki huduma za kibingwa ambazo zinaanza kutolewa leo katika hospitali zao, ili kupata ujuzi kutoka kwa madaktari bingwa waliotoka maeneo mbalimbali nchini. Hali hii itawawezesha kuendelea kusaidia wagonjwa pindi madaktari bingwa watakapoondoka.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Prisca Kayombo, wakati akipokea timu ya madaktari bingwa 36 wanaokwenda kutoa huduma za kibingwa katika hospitali za halmashauri mkoani humo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi